Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MZEE WA UPUPU: Bodi ijifunze hapa

Nahodha Wa Croatia, Luka Modric.jpeg Nahodha wa Croatia, Luka Modric

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kombe la Dunia 2022 limeshuhudia wachezaji wakubwa wote wakiwalalamikia waamuzi. Messi alimlalamikia mwamuzi dhidi ya Uholanzi, Antonio Mateu Lahoz, kwa maneno makali sana.

FIFA has to review that, it can’t give a referee like that a match of this importance, when they’re not up to the task.”

-FIFA lazima ipitie upya hiyo, hawawezi kumpa mwamuzi kama yule mechi muhimu kama ile, ilhali hayuko tayari kwa jukumu hilo.

Naye kipa wa Argentina, Emiliano Martinez, alisema

“I hope we don’t have that referee any more. He is useless.” -Natumaini hatuwi tena na mwamuzi huyo. Hana maana kabisa.”

Huu ulikuwa mchezo wa robo fainali na Argentina ilishinda na kutinga nusu fainali iliyowakutanisha na Croatia na kushinda 3-0.

Baada ya mchezo huo, nahodha wa Croatia, Luka Modric, akamlalamikia mwamuzi kwa maneno makali akimlaumu kwa penati iliyoipa Argentina bao la kwanza.

“I donít like to talk about referees but this is one of the worst. I donít have a good memory of him, he ís a disaster. For me it wasnít a penalty.”

-Sitaki kuongelea waamuzi lakini huyu ni mmoja kati ya waamuzi wa hovyo zaidi. Sina kumbukumbu naye, huyu ni majanga. Kwangu ile haikuwa penati.

Haya ni maneno makali sana lakini FIFA haikuchukua hatua zozote dhidi yao. Zaidi walikuwa waungwana, wakachutama. Maana wahenga wanasema muungwama akivuliwa nguo, huchutama. FIFA ikachutama na kuchukua hatua dhidi ya waamuzi.

Sasa rudi hapa nyumbani. Hawa wote wangefungiwa miezi mitatu. Bodi ya Ligi na kamati yake ya uendeshaji na usimamizi wa ligi hawataki kabisa mtu alalamike kuhusu waamuzi.

Kulalamika ni kupunguza machungu hasa baada ya kuumizwa. Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Alamsi Kasongo, alikuwa mchezaji na aliwahi kumpiga refa baada ya kutoridhishwa na uamuzi.

Siyo kwamba alichokifanya ni sahihi, hapana...ila angalau anaweza kuelewa hisia zinapokuwa pale damu inapochemka halafu unadhulumiwa haki yako.

Ukichunguza kwa makini utaona wote waliofungiwa kwa kulalamika baada ya mechi hawakututimia maneno makali kama ya Messi, Martinez na hata Luka Modric.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, baada ya sare tasa dhidi ya Newcastle United, alimlalamikia mwamuzi kwa kutowapa penalti mbili ambazo yeye alidhani ni halali.

“There were two penalties. It’s very simple. I’m talking about what I’ve seen. It was two scandalous penalties.”

-Kulikuwa na penalti mbili. Ni rahisi kabisa. Ninaongea kuhusu kile nilichokiona. Zilikuwa penalti mbili za kushangaza.

Labda Kiswahili kinaweza kuwa kimepunguza ukali wa maneno aliyotumia, au tafsiri yangu ikawa imekosa neno sahihi la neno SCANDALOUS.

Hili ni neno kubwa zaidi ya KUSHANGAZA kama nilivyotumia kwenye tafsiri. Scandalous inatokana na scandal yaani kashfa. Ukizidi kulichambua hili neno utaona Arteta alitumia kauli nzuri sana. Lakini Bodi ya Ligi ya England wala haikuwa na habari naye...kwa sababu ameongea ukweli.

Kimsingi sheria zote za mpira duniani zinakataza kuwakosea heshima waamuzi,.lakini siyo kuelezea hisia zako baada ya kutoridhishwa.

Wasimamizi wa mpira duniani wanajua mpira husababisha vimeng’enyo vya adrenaline kumwagika kwa wingi kwenye mishipa ya wahusika wakati wa mchezo.

Vimeng’enyo hivi ndiyo hupelekea matendo ambayo mtu hawezi kunuzuia nayo. Hiyo ni sayansi, na wenzetu wote wanajua kasoro sisi wa Bodi ya Ligi Tanzania. Wenzetu hupima madhara ya maneno ambayo mtu ameyasema baada ya mchezo, siyo tu kulalamika.

Kulalamika ni sehemu ya kujipoza maumivu hasa yaliyosababishwa na watu wengine waliotakiwa kuwa sehemu ya haki. Mlakamikaji akienda mbali hadi kumkosea heshima mwamuzi kama binadamu, hiyo siyo sawa.

Hapo ndipo mamlaka huingilia kumrudisha kwenye mstari...lakini siyo kusema mwamuzi hakuwa sahihi kwenye tukio fulani, basi ‘miezi mitatu’, hapana.

Bodi ya Ligi na TFF ijifunze kutoka huku, isiishie tu kusisimkwa na hisia za kishabiki, bali waangalie na namna wenzao wanaokalia viti kama vyao wanafanya nini.

Wanapaswa kutenda haki kwa kuzingatia na kuheshimu mawazo ya wale wanaozungumza sio kukurupuka kwa mihemko na kuwafungia na kuwapiga faina watu walioumizwa na kuwanyima uhuru na haki ya kusema. Mpira ni mchezo wa hadharani sio chumbani.

Chanzo: Mwanaspoti