Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MZEE WA MCHANGANI: Pogba apiga hat trick, anyimwa mpira

Pogba Mchangani Soka la Mchangani

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Hizo sheria ni zenu, huku kwetu hatuzijui” hiyo ni sauti za Simon Juma nahodha wa Malimbe FC, Mwanza baada ya kugoma kumpa mpira Rashid Shaban ‘Pogba’ wa Masha Boys baada ya kupiga hatrick kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika kwenye Uwanja wa Fitina juzikati.

Katika mchezo huo uliofanyika asubuhi bila mashabiki, Pogba alifunga hattrick na kuisaidia timu yake kushinda mabao 3-1 dhidi ya Malimbe FC, walikuwa wenye mpira.

Masha Boys walifika uwanjani hapo bila mpira na kulazimika kutumia mpira mmoja wa Malimbe.

Kwa kuwa kina Pogba wa Ulaya wakifunga Hattrick wanaondoka na mpira sasa na Pogba wa Masha akahisi yupo Ulaya na kutaka kupewa mpira na kujikuta akiambulia maneno ya kejeli namna hii;

“Wewe Pogba gani unacheza mchangani, hizo sheria ni zenu, huku kwetu hatuzijui. Yaani tukupe mpira wetu kwa lipi hasa? Thubutuu.”

Kwanza kibongo bongo hata kwenye Ligi ile wanayocheza kina Aucho na Bwalya hawapewi mipira sembuse wewe wa huku maporini?” amesema Juma kwa kejeli.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz