Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MO Dewji ateua wajumbe wanne Bodi ya Wakurugenzi Simba SC

Mo Dewji Bodi Mpyaaaaaaa MO Dewji ateua wajumbe wanne Simba

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwekezaji na Rais wa Heshimawa wa Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji 'Mo Dewji' amefanya uteuzi wa wajumbe wanne watakaoingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo kuungana na wajumbe wa kuchaguliwa wa upande wa wanachama.

Wajumbe hao ambao Mo amewateua chini ya Mwenyekiti, Salum Abdallah Muhene 'Try Again' ni Dkt. Raphael Chegeni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Mhe. Rashid Shangazi.

Hatua hiyo inafuatia kufanyika uchaguzi mkuu uliomrejesha madarakani Mwenyekiti Murtaza Mangungu na Wajumbe Dk. Seif Ramadhan Muba, Asha Baraka, CPA Issa Masoud Iddi, Rodney Chiduo na Seleman Haroub.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live