Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MO Dewji: Simba hatukati tamaa

MO Dewji: Simba Hatukati Tamaa MO Dewji: Simba hatukati tamaa

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa heshima wa Klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji 'MO' amewaambia mashabiki wenzake wa klabu hiyo kwamba wasikate tamaa licha ya kupoeteza dhidi ya Raja Casablanca wikiendi iliyopita.

MO amesema, mashabiki wa kweli huwa wanakuwa pamoja na timu kwenye nyakati zote, ziwe nzuri au mbaya.

“Simba, tunashinda pamoja, tunafungwa pamoja. Hatu kati tamaa. Tutaendeleza mapambano!,” Mo Dewji Muwekezaji wa Klabu ya Simba SC.

Simba anatarajia kushuka dimbani tena kesho kwenye Ligi Kuu ya NBC ambapo atavaana na Wanalambalamba wa Azam FC kisha atafunga safari kwenda Uganda kuwafata Vipers mechi ya Klabu Bingwa itakayochezwa Jumamosi Februari 25, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live