Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MEDDIE KAGERE: Mashabiki Simba tulieni, mambo matamu yanakuja

Meddie Kagere Scored For Simba Sc Vncm1722tkk41dxt5oibu2psh MEDDIE KAGERE: Mashabiki Simba tulieni, mambo matamu yanakuja

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

WIKI iliyopita tulipata ushindi wa kwanza ugenini katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwafunga wenyeji wetu, AS Vita ya nchini DR Congo.

Miongoni mwa sababu ambazo zilitusaidia kupata ushindi katika mchezo huo ni uzoefu wa mashindano ambao tumeanza kuwa nao.

Nakumbuka mara ya mwisho mpaka tunafika kwenye hatua ya robo fainali misimu miwili iliyopita tulikuwa na matokeo mabaya katika mechi zote tatu za ugenini.

Tulifanikiwa kufuzu kwenye hatua ya robo fainali kwa faida ya kucheza vizuri mechi za nyumbani, lakini ugenini tulikuwa vibaya.

Wakati tunacheza mechi hizo za ugenini licha ya kupata matokeo mabaya tulikuwa tunajifunza mambo mengi na kuna ambayo tumeanza kuyatumia msimu huu.

Wakati huo tulikuwa na ugeni wa mashindano kwani hatukuwahi kufika kwenye hatua kubwa kama hiyo katika mashindano haya makubwa kwa ngazi barani Afrika.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz