Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAYELE: Naweza kufunga kwa mitindo mingi

FISTON MAYELE MAYELE: Naweza kufunga kwa mitindo mingi

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

JANA katika makala haya supastaa mpya wa Yanga, Fiston Mayele aliyetua na kushtua mapema tu nchini kwa kuwapiga Simba kidude kwenye mchezo wa ngao ya jamii alizungumzia mambo mbalimbali. Ungana nasi katika hitimisho la makala hii.

WAKONGOMANI SITA YANGA

Msimu huu Yanga ina wachezaji sita Wakongomani kikosini ambapo kuna baadhi ya watu wanaamini hiyo haipo sawa, lakini Mayele ana mtazamo tofauti. Wachezaji hao ni Tonombe, Makambo, Djuma Shaaban, Jesus Moloko, Yanick Bangala na Mayele mwenyewe.

“Kwanza ni furaha kuona mnakutana na watu ambao mnatoka taifa moja, sijaona kama kuna ubaya jambo zuri kwetu ni kama linatupa presha ya kutakiwa kuonyesha kazi nzuri hapa Yanga. Watu wa hapa naambiwa wanawawwaamini watu wa Congo na tumeona wapo (wachezaji) ambao walikuja hapa na walifanikiwa zaidi mfano ni (Tuisila) Kisinda na Makambo,” anasema Mayele.

“Angalia Mukoko (Tonombe) wengi tulidhani kwamba akija Tanzania atapotea na kutoitwa tena timu ya taifa, lakini amekuja huku amefanya kazi na sasa anacheza timu ya taifa. Hiyo inatupa kazi ya kutakiwa kufanya kazi hapa ili watu wa Yanga wafurahie kazi yetu hapa. Wanaosema hii itakuwa mbaya kwa Yanga hawajui mpira na sisi tutafanya kazi kubwa hapa kuwapinga.

“Tunajua kwamba siku Yanga ikifungwa wako wataona hawa wachezaji wa Congo hawafai na sisi tunataka kuhakikisha inashinda, tutaweka nguvu kubwa katika kila mechi ili Yanga ifanye mazuri hapa Tanzania.”

MKATABA WAKE

Kuhusu mkataba wake Yanga, staa huyo ansema: “Nimesaini mkataba wa miaka miwili, nitakuwa hapa kwa muda huo mashabiki wa Yanga nawapenda sana. Wanapenda wachezaji wao, ningependa kubaki hapa muda zaidi kutokana na maisha ya hapa, lakini kama nitafanya vizuri na klabu nyingine itanihitaji utakuwa ni uamuzi wa uongozi, ila hii Yanga ni sehemu nzuri kwangu.”

MZUKA MASHABIKI YANGA

Akiwazungumzia mashabiki wa timu hiyo, anasema wamekuwa wakimfanya ajisikie vizuri kila kmara.

“Mashabiki wa Yanga nawapenda sana, wana kelele. Hata kama unatoka ukiwa umepoa unalazimika kuchangamka, ile hali naipenda sana ni kama mashabiki wa Vita wanakufanya mchezaji kuchangamka na kupambana zaidi, zile kelele ni kitu kizuri kwa wachezaji wanapokuwa uwanjani.”

BABA WA WATOTO WAWILI

Mayele ni mume na baba wa watoto na hapa anasema: “Nina familia, mke na watoto wawili. Mtoto wangu wa kwanza ana miaka mitatu anaitwa Maelle Kalala, lakini mwingine ni Manel ana miezi minne na wote ni wa kike.”

MITINDO YA KUFUNGA

Mchezaji huyo anasema katika kutupia mabao anaweza kufunga popoteza. “Nina mitindo mingi ya kucheza, naweza kufunga kwa mitindo mingi. Kwa kichwa na miguu, inategemea nimepokeaje mpira. Pia si mshambuliaji wa kusubiri nipewe (mpira) naweza kutafuta mwenyewe. Nikitengenezewa nitafunga,”.

KIDOGO ATIMKIE MISRI

Wakati anataka kuja Yanga iliibuka ofa ya klabu ya matajiri wa Misri, Al Ittihad, lakini jamaa akachomoa na hapa anaeleza.

“Wakati Yanga wananifuata sikuwa na ofa nyingi, lakini baada ya ligi kumalizika na Yanga kunihitaji kuna ofa kubwa ilikuja kutoka Misri nilitamani zile pesa lakini kuna wakati heshima inatakiwa kutangulia,” anasema.

“Rais wangu anayenimiliki ni mtu ambaye ana heshima kubwa Congo na anaheshimiana sana na Injinia Hersi sikutaka kuharibu heshima ya watu niliona acha nikubaliane kuja Yanga.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz