Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#MAP: Mmoja aanzie benchi

Pacome Maxi Aziz Ki Mmoja aanzie benchi

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Max Nzengeli, Stephanie Aziz Ki na Pacome Zouzoua. Hawa wote nafasi zao halisi ni Viungo Washambuliaji (Attacking Midfielders) au kwa lugha rahisi unaweza kuita "Inside Ten".

Kazi kubwa ya Kiungo Mshambuliaji anapokuwa uwanjani ni kutengeneza nafasi kwa washambuliaji ikiwa ni pamoja na kufunga. Ni mara chache sana utamuona akijihusisha na kukaba wakati timu inapokuwa haina mpira.

Kwa nini? Kwa sababu Kiungo Mshambuliaji hucheza kwenye eneo la juu, nyuma kidogo ya Mshambuliaji wa Kati.

Kwenye Morden Football wachezaji wanaocheza kwenye nafasi hii ni wachache sana. Mfano huko Ulaya, kuna kina Kay Hevertz, Joao Felix, Gavi, Bruno Fernandes na hata Kelvin De Bruney.

Unapokuwa na wachezaji watatu wanaocheza nafasi moja ya Kiungo Mshambuliaji kama ilivyo kwa Yanga, kitu kizuri utakachopata kutoka kwao ni pale timu inapokuwa na mpira.

Wakishambulia kwa ku-drive mpira kwa kasi kutoka kwenye Back Line kwenda kwenye Final Third, Lakini inapofika wakati timu inatakiwa ikabe, ipokonye mpira, kama kocha hapo ndipo unapoulizwa maswali magumu.

Ukiitazama Yanga ya Gamondi ni wazuri sana wakati timu inashambulia. Tofauti na Yanga ya msimu uliopita ambayo ilikuwa bora sana kwenye eneo la kukaba.

Uwepo wa Mudathir na Aucho kwenye Kiungo cha Kukaba, Musonda na Moloko kwenye Wings za kulia na kushoto uliifanya timu iwe na speed inaposhambulia na hata inaposhambuliwa.

Nadhani Mwalim Gamondi anapaswa kufanya maamuzi magumu kwa kumuweka benchi mmoja kati ya wachezaji hawa watatu, na akubali kuzifungua winga kwa kuwapa nafasi wachezaji wenye kasi kama vile Jesus Moloko na Farid Musa au hata Kennedy Musonda.

Unapokuwa na mawinga halisi hasa wale wenye speend kama ilivyo kwa jesus Moloko, kwanza inasaidia kuchosha mabeki wa pembeni wa timu pinzani na kuwazuia kupanda mara kwa mara.

Pili, timu inapata nafasi ya kushambulia kwa haraka wakiwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye eneo la wapinzani. Tatu, inasaidia ku-maintain energy ya timu, kwani mchezaji mmoja kati ya hawa anapochoka au kuumia unakuwa na SUB yenye quality ile ile ya wachezaji walioanza kwenye first eleven.

Wananchi...!!! Nadhani mpaka hapo tutakuwa tumeelewana?! Sasa kazi kwenu, mwambie Mwalim Gamondi apate huu udambwi udambwi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live