Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#MAKUNDICAF: Simba amepangwa kundi la kulipa kisasi - Jemedari

SAID JEMEDARI 1140x640 #MAKUNDICAF: Simba amepangwa kundi la kulipa kisasi - Jemedari

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka nchini Jemedari Said amesema, Simba ameapangwa kundi na timu mbili ambazo amekutana nazo miaka ya karibuni hivyo itakuwa ni mechi ya kisasi.

Baada ya droo ya Klabu Bingwa Afrika kuchezeshwa jioni hii Oktoba 6, 2023 na Simba kupangwa kundi moja na Wydad Casablanca, ASEC MIMOSAS na Jwaneng Galaxy, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jemedari ameandika hivi:

"Safari ya Mnyama kwenda NUSU FAINALI inaanzia hapa, kisasi kwa Jwaneng na Wydad."

Simba alitolewa na Jwaneng Galaxy, mwaka 2021-22 katika raundi ya pili ya mtoano na msimu uliopita 2023-24, Wydad iliwatoa Simba SC kwenye mchezo wa robo fainali Klabu Bingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live