Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAKOCHA 45 WAOMBA KAZI YANGA, MASTAA WATATU KUFYEKWA

Kazi Pic Data MAKOCHA 45 WAOMBA KAZI YANGA, MASTAA WATATU KUFYEKWA

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Khatimu NahekaMore by this Author YANGA ilitumia dakika zisizozidi 15 juzi usiku kumfuta kazi Kocha Cedrick Kaze. Waliingia tu hotelini wakakutana dakika chache wakakubaliana kumuita na kumtakia kila la heri kisha wakafuata wasaidizi wake kwa staili hiyo.

Uongozi umethibitisha kwamba kabla ya wikiendi watakuwa wameshapata Kocha Mkuu lakini Mwanaspoti linajua kwamba kuna wazawa wawili na Mkenya mmoja wanachuana vikali kupewa jukumu la kusimamia kwa muda.

Kabla ya mabosi wa Yanga hawajaenda kula jana walishapokea majina ya Makocha 45 wakiomba kazi lakini wamekubaliana timu itakaa chini Adolf Rishard(Kocha wa zamani wa Prisons) au Mecky Maxime(Kocha wa zamani wa Kagera) ambao ni wazawa pamoja na Mkenya, Ben Mwalala(Kocha wa zamani wa Bandari) ambaye ni straika wa zamani wa Yanga aliyewafutia uteja kwa Simba katikati ya miaka ya 2000.

Licha ya kwamba Yanga wamekuwa wasiri kuweka wazi majina kwa madai kwamba hawajamalizana nao lakini Mwanaspoti limepenyezewa kwamba watatu hao yoyote anaweza kula shavu kwavile wanaijua vilivyo Yanga.

Taarifa za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba Yanga inataka kuanza na kocha ambaye anaijua klabu hiyo kwa ndani au ligi ya Tanzania ingawa hata uwezekano wa Juma Mwambusi kurudi bado ni mkubwa kwani inaelezwa yupo Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga Dominic Albinius ameliambia Mwanaspoti kwamba wanataka mchakato huo kumalizika haraka ndani ya wiki moja.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz