Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MABADILIKO: Mechi ya Simba Vs Coasta Unioni kupigwa Uhuru

MABADILIKO: Mechi Ya Simba Vs Coasta Unioni Kupigwa Uhuru.jpeg MABADILIKO: Mechi ya Simba Vs Coasta Unioni kupigwa Uhuru

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya jana kuwepo kwa taarifa kuwa huwenda Wekundu wa Msimbazi Simba SC, watakipiga na Coastal Union katika uwanja wa Azam Complex, taarifa mpya ni kwamba mbungi itacheza katika dimba la Uhuru.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kutangaza hivi:

"Mchezo wetu wa ligi kuu NBC dhidi ya Coastal Union utapigwa kesho katika dimba la Uhuru Jijini Dar Es Salaam Saa 10:00 jioni."

Awali, Ahmed alinukuliwa akisema walikuwa kwenye mazungumzo ya kutafuta uwanja mwingine badala ya Uhuru lakini hata hivyo bila shaka ilishindikana kwani uwanja waliokuwa wanauwinda (Azam Complex) wenyewe Azam FC nao wana mechi kesho dhidi ya Singida BS.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live