Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lyon yaingia vitani dhidi ya Man U kumuwania Benzema

Benzema Ahusishwa Na Ugaidi Karim Benzema

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Olympique Lyon inafanya mazungumzo na Al-Ittihad ili kumrudisha mshambuliaji wa timu hiyo Karim Benzema, 36, ikiwa ni baada ya zaidi ya miaka 14 tangu alipoondoka 2009 kwenda Real Madrid.

Kuanza kwa mazungumzo Lyon kunaifanya iingie kwenye vita dhidi ya timu mbalimbali ambazo pia zinamnyemelea ikiwa ni pamoja na Manchester United.

Benzema ambaye amesimamishwa na Al-Ittihad baada ya kuchelewa kujiunga na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu anaweza kuwa mchezaji mwingine maarufu kuondoka Saudi Arabia baada ya Jordan Henderson.

Mazungumzo juu ya dili hilo tayari yameshaanza ingawa inaonekana kuwa haitakuwa rahisi kumsajili kwa sababu ya mshahara mkubwa anaoupata kwenye kikosi chake cha sasa.

Taarifa zinadai Lyon inataka kumsajili kwa mkopo, hivyo kutua kwake itategemea na makubaliano ya malipo ya mshahara juu ya timu hizo.

Benzema, 36 alitua Ittihad majira ya kiangazi 2023/24.

Chanzo: Mwanaspoti