Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lyanga ndoto yangu ni kucheza na Nyoni timu moja

58929 Pic+lyanga

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Kinara wa mabao wa Coastal Union, Ayub Lyanga ametaja mchezaji wake bora msimu huu ni beki kiraka wa Simba, Erasto Nyoni na anatamani siku moja acheze naye timu moja.

Lyanga amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Coastal Union, alisema Nyoni ni mwalimu wa soka mbali na uchezaji wake anapenda kucheza kwa maelekezo.

Alisema tangu ameanza kucheza soka la ushindani amekuwa akivutiwa na soka la mchezaji huyo na kuomba Mungu siku moja aweze kucheza naye katika timu moja huku akiamini kuwa atakama siyo katika ligi basi wanaweza kukutana katika kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars'.

"Bado nina mkataba mmoja na Coastal Union na hadi sasa bado sijapokea ofa yoyote kutoka kwa timu yeyote, lakini nina imani ipo siku nitacheza timu moja na Nyoni na nitaweza kujifunza mengi kutoka kwake kwani ni mtu ambaye nimekuwa nikimfuatilia kwa muda mrefu,"

"Hakuna lisilo wezekana sisi sote ni Watanzania na tuna timu moja ambayo kila mchezaji anapata nafasi ya kucheza kutokana na ubora anaouonyesha kwa wakati katika timu yake hivyo kama nitashindwa kucheza na Nyoni timu moja ya ligi basi tunaweza kukutana Stars," alisema Lyanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz