Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lyanga asaini miwili Simba

Lyanga Lyanga asaini miwili Simba

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Klabu ya Azam FC kutoa Thank You kwa wachezaji wake wanne ambao walikua wanaitumikia klabu hiyo msimu uliomalizika na wengine walikua kwa mkopo vilabu vingine. Mmoja wapo alikuwa ni Ayoub Lyanga.

Taarifa za kuaminika kutoka Kwa mtu wa karibu wa Ayoub Lyanga, amesema kuwa Mchezaji huyo amemalizana na Simba.

Lyanga amesaini miaka miwili ya kutumikia timu hiyo, huku ikielezwa hiyo ndiyo Sababu ya kugomea mkataba mpya wa kuendelea kubaki Azam FC.

Lyanga aliagwa Jana na Azam FC ambao amewatumikia kwa misimu takribani minne, kabla ya hapo nyota huyo alikuwa anaitumikia Coastal Union.

Azam FC pia waliachana na wachezaji wao wengine kama, Charles Edward Manyama, Issa Ndala, pamoja na Malickou Ndoye hawa wachezaji watakua sio sehemu ya kikosi cha matajiri hao wa jiji la Dar-es-salaam kuelekea msimu wa 2024/25.

AZAM FC wanafanya usajili wa nguvu ambao utawapa nafasi ya kufanya vizuri katika ligi kuu ya NBC, Lakini pia kufanya vizuri kimataifa kwani msimu ujao watacheza ligi ya mabingwa barani Afrika hivo hawataki kutia aibu kabisa.

Wana Rambaramba wamepanga kufanya maboresho makubwa sana katika kikosi chake kuelekea msimu ujao ushindani ambao wameutoa kwenye ligi ya NBC msimu uliomalizika na kumaliza nafasi ya pili hawajaridhidshwa nao, Kwani kwa msimu ujao wanaamini kama wataboresha kikosi chao basi wanaweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live