Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lwanga ndio basi tena Simba, Bwalya atajwa

Lwanga Simba.jpeg Thadeo Lwanga

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaambiwa mwenendo wa majeraha kwa kiungo Taddeo Lwanga raia wa Uganda, umemfanya Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco alazimike kumuongeza mkataba mpya kiungo wake raia wa Zambia, Rally Bwalya.

Bwalya alisajiliwa Simba Agosti 15, 2020 akitokea Power Dynamos FC ya kwao Zambia, huku usajili wake ukizua taharuki kubwa kwa watani wao Yanga, ambapo tayari ameshaonyesha uwezo mkubwa ndani ya kikosi hicho jambo ambalo linamfanya Pablo kumuombea mkataba mpya.

Chanzo cha kuaminika kutoka Simba kimesema kwamba, pamoja na mkataba wa Bwalya kutarajiwa kuisha katikati ya msimu huu, majeraha ya Lwanga yameufanya uongozi huo kulazimika kumuongeza mkataba ili aweze kusaidiana na kiungo mkabaji atakayekuja kuchukua nafasi yake.

“Kuna wachezaji wengi wanatarajiwa kuachwa mwishoni mwa msimu huu na mmoja wapo ni Lwanga, ambaye hali yake ya afya imeshakuwa ya kutisha tangu alipofanyiwa upasuaji, hivyo uongozi umelazimika kumbakiza Bwalya ndani ya timu ili kulainisha safu hiyo ya kiungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live