Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lwanga Injini isiyoimbwa Simba

Lwanga Pic Data Lwanga Injini isiyoimbwa Simba

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author MASHABIKI wa klabu ya Simba kwa sasa hata akosekane kiungo wao mahiri, Jonas Mkude hawana presha na hilo kutokana na kuwa na viungo imara katika nafasi hiyo.

Simba katika dirisha dogo ilimsajili kiungo Taddeo Lwanga ambaye baada ya kupata vibali vyake alianza kuvaa jezi za timu hiyo na kuonyesha uwezo bora anapokuwa uwanjani.

Uwepo wake kwenye dimba bila shaka umewafanya mashabiki wamsahau kimtindo Mkude ambaye alisimamishwa kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu.

Mwanaspoti limemuangalia kwa kina kiungo huyo na huu ni uchambuzi wa kina wa namna ambavyo anacheza pindi anapolipigania chama lake.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz