Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Luvanga anukia Marekani

Clara Luvanga Goals Clara Luvanga

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa kimataifa, Clara Luvanga anayekipiga Al Nassr ya Saudia huenda msimu ujao akaibukia Marekani baada ya kuanza mazungumzo na moja ya timu za nchini humo.

Ikumbukwe msimu uliopita, Al Nassr ilivunja mkataba wa straika huyo na Dux Lugrono ya Hispania ikiwa miezi mitatu tu asajiliwe huko. Nyota huyo bado ana mkataba wa miaka miwili na miamba hiyo ya soka ya Saudia na kuna ofa za timu tatu kutoka Marekani zinazotaka kuvunja mkataba na klabu hiyo ili kumnasa.

Akizungumza Clara alisema “Siwezi kutaja ni timu gani, ila muda ukifika mtajua lakini ni kweli ni timu kubwa Marekani zimenitafuta nami bado nina mkataba na Al Nassr, iwapo tutafikia makubaliano basi naweza kujiunga na moja wapo,” alisema Clara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live