Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lusajo, Kichuya wakabidhiwa rungu...Mayele ndani

Namungo Strikers.jpeg Washambuliaji wa Namungo

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Waahambuliaji Reliants Lusajo na Shiza Kichuya wa Namungo wanaongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga utakaochezwa saa 1:00 usiku katika uwanja wa Majaliwa.

Kichuya anakumbukwa msimu uliopita kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Mkapa, alifunga bao la kufutia machozi wakati Namungo ikifungwa 2-1 mabao yaliyofungwa na Fiston Mayele sambamba na Feisal Salum.

Wachezaji wengine wanaoanza katika mchezo huu ni Jonathan Nahimana, Emmanuel Asante, Hashim Manyana, Christoper Oruchum, Frank Magingi na Hamis Nyenye.

Wengine ni Jacob Masawe, Seidou Blandja na Lucas Kikoti.

MAYELE NDANI

Wakati huohuo upande wa Yanga, mshambuliaji Fiston Mayele amerejea kwenye kikosi baada ya kukosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kuelezwa ni majeruhi.

Mayele atakuwa sambamba na Aziz Ki kwenye eneo la ushambuliaji kuhakikisha wanapeleka mashambulizi langoni kwa Yanga.

Beki Dickson Job pia amerejea baada ya kumaliza adhabu yake ya kadi tatu za njanoo na kukosa mchezo dhidi ya Prisons.

Kikosi kinachoanza ni Diara Djigui, KibwanShomari, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Yanicka Bangala na Khalid Aucho.

Wengine ni Feisal Salum, Jesus Moloko (amerejea kikosini), Aziz Ki na Tuisila Kisinda.

Chanzo: Mwanaspoti