Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lule amuomba msamaha Nabi

Nabi Pic Data (600 X 326) Lule amuomba msamaha Nabi

Sun, 6 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baada ya kuzinguana kwa dakika kadhaa makocha wa Yanga Nasreddine Nabi na yule wa Mbeya City Mathias Lule wameyamaliza kwa kuombana msamaha.

Tukio la makocha hao kutofautiana lilijiri katika dakika za mwisho kwenye mchezo baina ya timu hizo uliopigwa jana usiku Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Almanusura makocha hao washikane mashati kama sio kuamuliwa kufuatia kupishana kauli mara baada ya firimbi ya mwisho ya mchezo Nabi akionekana kukerwa na kitu kutoka kwa Lule.

Hata hivyo mara baada Lule kutoka katika mkutano wa wanahabari alionekana kumtafuta Nabi kisha kukutana na msaidizi wake daktari wa viungo Youssef Mohamed.

"Rafiki naomba umwambie kocha (Nabi) kwamba namuomba radhi kwa kile kilichotokea hatutakiwi kuishi hivi nifikishie ujumbe huu kwake kwamba nimemuomba radhi," alisikika Lule akiongea na Mohamed.

Akizungumza baada ya kupokea ujumbe huo Nabi amesema amemsamehe Lule kwa kile kilichotokea na wala hana kinyongo naye tena.

"Ndio, niliambiwa kwamba ameniomba radhi nadhani aliona kwamba hakufanya kitu sahihi na nimemsamehe sina tatizo na mtu na sio kwasababu nimepata sare kilichotokea ilikuwa ni suala la mtu kumuheshimu mwenzake," amesema Nabi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz