Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukula: Nitabadili Kikosi cha Kwanza

Charles Lukula  SQ Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba Queens, Charles Lukula

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba Queens, Charles Lukula amesema kuwa kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi atabadilisha kikosi cha kwanza.

Simba Queens walifanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye mashindano hayo juzi jumatano baada ya kuichapa Determine Girls kwa mabao 2-0.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Lukula alisema “Wapinzani wetu walikuja na mbinu ya kutoruhusu mabao.

“Wachezaji wangu walikuwa na presha kubwa kwa kutaka kupata matokeo lakini tulivyoenda vyumbani niliwatuliza na kuongea nao hivyo walivyoingia kipindi cha pili waliweza kufunga mabao.

“Nitafanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza kwani kuna watu ambao hawatoi kile ambacho tunakifanya mazoezini kitu ambacho kinasababisha umakini mdogo wa kupata matokeo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live