Kocha na mchambuzi wa kituo cha radio cha Efm, Tigana Lukinja amefunguka mara baada ya beki kisiki wa Simba ambaye ni raia wa Kenya, Joash Onyango kuondoka klabuni hapo na kujiunga na Singida Fountain Gate.
"Kama ni kweli Joash Onyango kaondoka Simba SC basi kuna pengo kaliacha, lakini Singida wamelamba dume"
"Sisi walimu tunafundishwa, katika kitu ambacho huwa hatutakiwi kukibomoa kwa haraka ni Defense. kwa nini ?!"
"Wachezaji wageni hata kama ni wazuri huwa wanachukua muda ku-adapt mazingira mapya japo sio wote. Wakati mchezaji mpya anaendelea kuzoea mazingira mapya unapaswa kuwa na mchezaji mwingine ambaye ni mzoefu kwenye eneo hilo"
"Mfano ; Simba walimsajili beki mzuri tu, tena alitoka kucheza Champions league, Ouatarra ili aje achukue nafasi ya Onyango"
"Kwenye mechi yake ya (1) tu ya mashindano ambayo walicheza pacha na Inonga, Ngao ya hisani, Mayele alikuwa anawageuza tu atakavyo, anamwambia Aziz Ki, weka hapa, Simba wakapoteza mechi"
"Mazingira mapya yalifanya Ouatarra ashindwe ku-cop haraka ikabidi Onyango mzoefu arejee kikosini, na akacheza mara nyingi zaidi (Regular starter) kuliko beki yoyote"
"Unadhani asingekuwepo ingekuwaje ? Ikumbukwe pia, Simba ndio timu iliyoruhusu magoli machache zaidi ligi kuu (17), Yanga (18), miongoni mwa waliounda ukuta huo imara ulioruhusu magoli machache ni Onyango"
"Kama ni kweli kaondoka tuombe Mungu beki mpya huyo bwana mdogo anayetajwa asipate changamoto za ugeni, ku-adapt mazingira mapya na ku-cop na wenzie," amesema Tigana Lukinja.