Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku ni wa moto huko

Romelo Lukaku AS Roma Lukaku ni wa moto huko

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Ubelgiji, Romelu Lukaku aliifungia timu hiyo magoli manne katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Azerbaijan kwenye mechi za kufuzu EURO 2024 na kukwea kileleni mwa msimamo wa wafungaji bora michuano ya kufuzu EURO 2024 akiwa na magoli 14.

VINARA WA MAGOLI KUFUZU EURO 2024

1. Lukaku — 14

2. Ronaldo — 10

3. Mbappé — 9

4. Kane — 8

5. Højlund — 7

5. McTominay — 7

Lukaku ameendelea kujichimbia kileleni mwa ufungaji bora wa timu ya Ubelgiji akifikisha magoli 83 katika mechi 113 akiwa mbele kwa magoli 50 mbele Eden Hazard (mechi 125, magoli 33) anayemfuatia.

Aidha Lukaku anakamata nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote kimataifa kutoka Ulaya nyuma ya Cristiano Ronaldo na Ferenc Puskas.

VINARA WA MAGOLI WA MUDA WOTE ULAYA KIMATAIFA

Ronaldo — 127

Puskas — 84

Lukaku — 83.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live