Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku naye nje Kombe la Dunia Qatar

B7b2768a 9c53 43bd B76c 0e4c48ebb6ca Lukaku

Sun, 20 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vipigo vya majeraha vinaendelea kwa baadhi ya timu za taifa huku habari kuwa mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku hataichezea Ubelgiji kwenye Kombe la Dunia hadi angalau mechi yao ya mwisho ya Kundi F dhidi ya Croatia, kwa mujibu wa AFP.

Mshambuliaji huyo hakushiriki katika mazoezi ya kwanza ya timu hiyo tangu walipowasili Qatar siku ya Ijumaa huku akiendelea kupata nafuu kutokana na jeraha la misuli ya paja.

Ameichezea Inter mara mbili pekee tangu Agosti baada ya kupata jeraha katika kipigo cha 3-1 dhidi ya Lazio.

Lukaku alifunga ushindi wa 4-0 dhidi ya Viktoria Plzen ambao uliihakikishia Inter kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa lakini kisha akaumia msuli wake wa paja tena siku chache baadaye.

Ubelgiji wataanza kampeni zao za Kombe la Dunia Jumatano dhidi ya Canada na pia kumenyana na Morocco kabla ya kukipiga na Croatia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live