Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku kusepa Chelsea, ampiga chini wakala wake na kujipeleka kwa Mino Raiola

Tuchel With Lukaku 22.png Lukaku

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Chelsea ambao ni Mabingwa wa Ulaya kwa ngazi ya vilabu Romelu Lukaku anafikiria uamuzi wa kubadili wakala wake ili kutengeneza mazingira ya kuhama katika klabu hiyo yenye maskani yake jijini London.

Wakala wa sasa wa Romelu Lukaku anaitwa Federico Pastorello ambaye anataka kumbadili ili amchukue Mino Raiola ambaye ni moja ya mawaka bora kwa sasa Barani Ulaya.

Mino Raiola ana uhusiano mzuri na Mkurugenzi wa Michezo wa Klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa ambayo ndiyo inahusishwa na kuitaka saini ya Romelu Bolingoli Lukaku.

Lukaku amekuwa na wakati mgumu tangu ajiunge na klabu ya Chelsea akitokea Inter Milan ambapo amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara lakini pia amekuwa akisugua benchi chini ya utawala wa Kocha Thomas Tuchel kwa kile kinachosemekana kuwa haendani na mfumo na falsafa za kocha huyo.

Lukaku alisajiliwa na Chelsea kwa Zaidi ya paundi milioni 93 huku aianza kwa moto baada ya kufunga magoli matatu kwenye mechi mbili za mwanzo kabla ya kuandamwa na majeruhi na aliporudi akawa amepoteza namba yake katika kikosi cha kwanza kutokana na kiwango kizuri cha mshambuliaji raia wa Ujerumani Kai Havertz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live