Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku kupigwa bei mazima AS Roma

Mourinho Lukaku Lukaku kupigwa bei mazima AS Roma

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Agosti 2021, Chelsea ililipa Pauni 97.5 milioni kunasa saini ya Romelu Lukaku arudi kwenye kikosi akitokea Inter Milan, lakini sasa imekubali kumpiga bei kwa Pauni 37 milioni tu aende zake AS Roma.

Straika Lukaku, ambaye kwa awamu zote mbili alizosajiliwa na Chelsea hakuna kitu amefanya cha maana na sasa wanapiga hesabu za kuachana naye jumla mwisho wa msimu kwa kuwauzia AS Roma jumla baada ya huu mkopo wake wa msimu huu utakapofika tamati.

Lukaku amekuwa hana wakati mzuri na Chelsea, ambaye walimrudisha baada ya kuona ametamba na Inter Milan na kuwapa ubingwa wa Serie A. Sasa imemrudisha tena kwa mkopo huko Italia, mahali ambako kunaonekana kuwa na upepo mzuri kwa straika huyo wa Kibelgiji.

Lukaku ameanza vyema maisha yake huko Roma, akifunga mabao saba katika mechi nane alizocheza kwenye michuano yote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live