Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku awindwa PSG

Lukaku Nyavu Straika wa Chelsea, Romelu Lukaku

Wed, 13 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Habari ndo hiyo. Paris Saint-Germain imeripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na straika wa Chelsea, Romelu Lukaku, kwa ajili ya kumvuta akakipiga kwenye kikosi hicho cha Ligue 1.

Straika huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, Lukaku, 28, amekuwa hana maajabu kwenye kikosi cha The Blues tangu alipojiunga kwa mkwanja mrefu, Pauni 98 milioni mwaka jana akitokea Inter Milan.

Kiwango chake cha hovyo ndani ya uwanja kimemfanya ajikute akose nafasi katika kikosi cha Thomas Tuchel, ambaye amekuwa akipendelea zaidi kumtumia kiungo Kai Havertz kama Namba 9 bandia.

Na Lukaku anafikiria kwenda kuanza upya huko Ufaransa ambapo wakala wake Mino Railo yupo kwenye mazungumzo na mkurugenzi wa michezo wa PSG, Leandro kufanikisha uhamisho huo kwa mujibu wa But!.

PSG inaweza kuwa na uhitaji mkubwa wa mshambuliaji wa kati baada ya kuwapo na uwezekano wa Kylian Mbappe kuondoka.

Mbappe mkataba wake huko PSG utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa na Real Madrid.

Lukaku amefunga mabao matano tu kwenye ligi msimu huu, lakini PSG wao hawajali wanamwona kuwa mtu sahihi wa kwenda kuchukua mikoba ya Mbappe.

Hata hivyo, kuna ripoti nyingine zinadai kwamba PSG wanafikiria kwenda kumnasa staa wa Ajax, Anthony na Amine Gouiri wa Nice, ambao wanaowaona watakuwa na gharama nafuu kuliko Lukaku. Chelsea inaweza kukubali kumwaachia Lukaku kwa mkopo ili kupunguza bili ya mishahara na wanafikiria kwenda kunasa huduma ya winga wa Barcelona, Ousmane Dembele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live