Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku awakutanisha Vigogo Inter Milan, Chelsea

Lukaku.jpeg Mshambuliaji wa Inter Romelu Lukaku

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa Chelsea wamewauliza Inter Milan ikiwa wanaweza kumjumuisha kiungo Nicolo Barella kama sehemu ya ofa ili wawauzie Romelu Lukaku katika dirisha hili.

Lukaku ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Inter ameweka wazi kwamba anahitaji kuendelea kusalia Inter Milan.

Chelsea ipo tayari kumwachia lakini kwa sharti la pesa ama mabadilishano ya wachezaji ambapo wanamhitaji sana kiungo Nicolo Barella.

Lukaku anajihisi mwenye furaha kuendelea kusalia Inter na haoni ikiwa atapata nafasi ya kucheza kama anavyopata sasa ikiwa atarudi Chelsea.

Chelsea imevutiwa sana na kiwango cha Barella alichoonyesha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na aliisaidia Inter kufika fainali.

Mkataba wa sasa wa Barella unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.Msimu uliopita alicheza mechi 52 za michuano yote, amefunga mabao tisa na kutoa asisti 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live