Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku arejeshwa kikosini Chelsea

Lukaku Arudi Lukaku amerejea kwenye mazoezi ya kikosi cha Chelsea

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuteka vichwa vya habari kwa wiki nzima, Bifu ya Romelu Lukaku vs Thomas Tuchel imefikia ukingoni. Yameisha!

Lukaku alifanya mahojiano na kituo cha Sky Sport Italia ambapo, mahojiano yale yalizua gumzo kwenye ulimwengu wa soka. Kufuatia ukubwa wa habari hiyo, mshambuliaji huyo aliondolewa kwenye hesabu za Tuchel kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.

Baada ya maongezi ya ana kwa ana kati ya Romelu na Tuchel, sasa yameisha. Tuchel amethibitisha kumjumuisha mshambuliaji huyo kwenye orodha ya wachezaji watakaochuana na Spurs wiki hii.

Chelsea watapambana na Spurs katika mchezo wa nusu fainali ya Carabao Cup. Huu ni mchezo muhimu kwa timu zote katika kujiweka kwenye nafasi ya kubeba kikombe msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live