Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku ajiweka njia panda, Ulaya au Saudia

Romelu Lukaku Roma Lukaku ajiweka njia panda, Ulaya au Saudia

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji Romelu Lukaku huenda akabadilisha upepo na kutimkia Saudi Arabia, baada ya mkataba wake wa mkopo AS Roma ya Italia kukamilikana alijiunga nayo akitokea Chelsea.

Lukaku amekuwa akihusishwa na taarifa za kuachana na Chelsea kipindi hiki cha usajili wa majira ya joto, huku vyombo vya habari vya Italia vikieleza SSC Napoli inajipanga kumsajili.

Hata hivyo, Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, amekiri kupendezwa na mazingira ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia, hali ambayo imedhihirisha huenda akaamua kuondoka Ulaya na kutimkia Mashariki ya Kati.

Mshambuliaji huyo kutoka Ubelgiji amesema Soka ni sehemu ya maisha yake na atakuwa tayari kucheza popote pale atakaporidhika napo, hivyo lolote linaweza kutokea katika kipindi hiki.

“Soka ni sehemu ya maisha yangu, nitapendelea kucheza popote pale, lakini jambo la msingi ni pale nitakapopapenda na kufurahia maisha ya huko. Saudi Arabia ni kuzuri na nimewahi kucheza huko.

“Nakumbuka nikiwa na AS Roma tulikwenda Riyadh na tulicheza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Al Shabab ya Yannick Carrasco.

"Mara nyingi nilizungumza na Yannick kuhusu maisha ya huko. Anaishi katika makazi mzuri, ana kila kitu huko."

Kuhusu mustakabali wake, Lukaku ambaye anahusishwa na SSC Napoli amesema: "Watu wengi wanapenda kuongea, labda kwa sababu sina wakala. Lakini nitaamua. Nina udhibiti wa hali yangu. Nitafanya uamuzi sahihi muda utakapofika.

“Angalia, kila nilipoamua kubaki au kuondoka mahali fulani, baadhi ya mambo, kwa mfano uhusiano wangu na kocha, yaligeuka kuwa chaguo sahihi.

Alipoulizwa kuhusu kocha bora ambaye amefanya kazi naye, amejibu: "Antonio Conte."Mshambuliaji Romelu Lukaku huenda akabadilisha upepo na kutimkia Saudi Arabia, baada ya kukamilisha mpango wa kuitumikia AS Roma ya Italia kwa mkataba wa mkopo akitokea Chelsea.

Lukaku amekuwa akihusishwa na taarifa za kuachana na Chelsea katika kipindi hiki cha Usajili wa majira Joto, huku vyombo vya habari vya Italia vikieleza SSC Napoli inajipanga kumsajili.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, amekiri kupendezwa na mazingira ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia, hali ambayo imedhihirisha huenda akaamua kuondoka Barani Ulaya na kutimkia Mashariki ya Kati.

Mshambuliaji huyo kutoka Ubelgiji amesema soka ni sehemu ya maisha yake na atakuwa tayari kucheza popote pale atakaporidhika napo, hivyo lolote linaweza kutokea katika kipindi hiki.

“Soka ni sehemu ya maisha yangu, nitapendelea kucheza popote pale, lakini jambo la msingi ni pale na nitapapenda na kufurahia maisha ya huko. Saudi Arabia ni kuzuri na nimewahi kucheza huko.

“Nakumbuka nikiwa na AS Roma tulikwenda Riyadh na tulicheza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Al Shabab ya Yannick Carrasco.

"Mara nyingi nilizungumza na Yannick kuhusu maisha ya huko. Anaishi katika makazi mzuri, ana kila kitu huko."

Kuhusu mustakabali wake, Lukaku ambaye anahusishwa na SSC Napoli amesema: "Watu wengi wanapenda kuongea, labda kwa sababu sina wakala. Lakini nitaamua. Nina udhibiti wa hali yangu. Nitafanya uamuzi sahihi muda utakapofika.

“Angalia, kila nilipoamua kubaki au kuondoka mahali fulani, baadhi ya mambo, kwa mfano uhusiano wangu na kocha, yaligeuka kuwa chaguo sahihi.

Alipoulizwa kuhusu kocha bora ambaye amefanya kazi naye, amejibu: "Antonio Conte."

Chanzo: Mwanaspoti