Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku aipa Inter ushindi mbele ya Porto

Lukaku Winning Goal.jfif Lukaku aipa Inter ushindi mbele ya Porto

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Romelu Lukaku akitokea benchi ameipa ushindi klabu yake ya Inter Milan baada ya kufunga bao pekee kwenye mchezo dhidi ya FC Porto mtanange wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora uliochezwa Jumatano, dimba la San Siro.

Kwenye dakika ya 86 Lukaku alipiga shuti ambalo liligonga mtambaa wa panya na kumrudia tena kisha kumalizia mpira huo na kuingia kambani.

Pengine usingekuwa ubora wa kipa Andre Onana, Porto waliomaliza mchezo wakiwa pungufu wangeweza kupata hata goli moja baada ya juhudi za Zaidu Sanusi na Mehdi Taremi kuishia mikononi mwake.

Otavio kwenye dakika ya 78 alitolewa nje ya uwanja kwa kuonyeshwa kadi mbili za njano na kupelekea kadi nyekundu.

Sasa matokeo hayo yanaifanya Porto kuhitaji ushindi kwenye mechi ya marudiano ambayo watacheza nyumbani dimba la Estadio Dragao Machi 14 ili kufuzu kucheza robo fainali ya Uefa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live