Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku : Sifurahishwi na hali ya Chelsea, Nitarejea Inter

SPORT PREVIEW Lukaku 2TTT Romelu Lukaku

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku amefunguka na kuweka wazi kutofurahishwa na mfumo unaotumika na meneja wake Thomas Tuchel ndani ya klabu hiyo.

Lukaku ameenda mbali zaidi na kusema hana furaha ndani ya klabu hiyo na ipo siku atarejea katika klabu ya Inter Milan kwani anajutia jinsi gani aliondoka ndani ya klabu hiyo.

” Utimamu wa kimwili nipo sawa . Lakini sina furaha na hali ilivyo ndani ya Chelsea. Tuchel ameamua kucheza na mfumo mwingine – sitokata tamaa , nitakuwa professional, sina furaha na hali ilivyo lakini nitakuwa professional na siwezi kukata tamaa sasa . “ alisema Lukaku.

“ Ni matumaini yangu kutoka moyoni kabisa kurejea tena Inter Milan tena sio mwisho wa maisha yangu ya soka bali bado nikiwa katika ubora wangu ili kutwaa zaidi mataji pamoja .

“Nataka kuomba msamaha kwa mashabiki wa Inter , muda ambao niliongea maneno yangu haukuwa muda sahihi , mulichonifanyia kitabaki milele kwenye moyo wangu “

“ Huu ni muda sahihi wa kushea hisia zangu , mara zote huwa nasema Inter ipo moyoni mwangu , najua nitarejea Inter Milan , naipenda Italia , huu ni muda sahihi wa kuongea na kuwafahamisha watu nini kilitokea “

“ Nafikiri kila kitu kilichotokea majira ya kiangazi yaliyopita , haikutakiwa kutokea kama vile …jinsi nilivyoondoka Inter , namna nilivyoondoka klabuni , jinsi nilivyowasiliana na mashabiki …inanisumbua kwasababu haikuwa muda sahihi “ aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live