Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukaku, Kepa kuitajirisha Chelsea

Lukaku, Kepa Lukaku, Kepa kuitajirisha Chelsea

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly anadaiwa kuwa kwenye mpango wa kuwauza mastaa wa timu hiyo Romelu Lukaku, 30, anayecheza kwa mkopo AS Roma na Kepa Arrizabalaga anayecheza kwa mkopo Real Madrid.

Tobby amepanga mastaa hawa wauzwe dirisha lijalo la majira ya kiangazi na timu kibao kutoka Saudi Arabia zimeshaonyesha nia ya kutaka kuwasajili.

Chelsea inawauza nyota hawa kwa sababu hawaonekani kuwa kwenye mipango ya Mauricio Pochettino kwa msimu ujao ikiwa na malengo ya kukusanya zaidi ya Pauni 100 milioni itakazotumika kufanya usajili dirisha lijalo.

Lukaku na Kepa waliondoka Chelsea dirisha lililopita la majira ya kiangazi ili kutafuta sehemu zitakazowapa nafasi kubwa zaidi ya kucheza. Mkataba wa Lukaku unamalizika mwaka 2026, huku ule wa Kepa ukimalizika mwaka 2025.

Akiwa na Roma, Lukalu ameichezea mechi 25 msimu huu na kuifungia mabao 10 na kuasisti mara tatu, huku kwenye michuano ya Europa League amecheza mechi tisa amefunga mabao saba na kuasisti moja na leo usiku atakuwa na nafasi ya kuongeza idadi ya mabao wakati timu hiyo itakaporudiana na Brighton iliyoifunga 4-0 katika mechi ya kwanza ikiwania kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: