Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Luka Modric hana mpango wa kustaafu

Luka Modric Retf Luka Modric

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa timu ya Taifa Croatia, Mkongwe Luka Modric amethibitisha kuwa hana mpango wa kutundika daluga kuchezea timu ya Taifa Croatia kwa sasa na kubainisha kuwa ataendelea kucheza mpaka walau michuano ya UEFA Nations League majira wa kiangazi mwakani.

Akizungumzia baada ya kuiongoza Croatia kushinda 2-1 dhidi ya Morocco na kushika nafasi ya tatu huku akichukua medali ya shaba Modric amesema:-

“Ndiyo, huenda huu ukawa mchezo wangu wa mwisho wa Kombe la Dunia, lakini siwezi kusema lolote. Lakini bila shaka, nina furaha sana kwa kazi yangu yote kwenye timu ya Taifa Croatia. Kushinda medali mbili ni muhimu sana, ndoto yangu ilikuwa kushinda Kombe lakini hatukufanikiwa,” amesema Modric

“Lakini nina furaha sana, tumethibitisha kwamba Croatia ina timu kubwa, yenye mustakabali mzuri sana mbele yetu na lazima tuendelee. Katika siku zijazo, tutaona kitakachotokea. Angalau nataka kuendelea hadi Ligi ya Mataifa ya Ulaya na ndipo tutaona kitakachotokea.” ameongeza Modric.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live