Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Luis Rubiales: Uchunguzi waanzishwa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia

Luis Rubiales: Uchunguzi Waanzishwa Kuhusu Unyanyasaji Wa Kijinsia Luis Rubiales: Uchunguzi waanzishwa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Uchunguzi wa ndani umeanzishwa na shirikisho la soka la Uhispania baada ya kifungu cha unyanyasaji wa kijinsia kuanza kufanya kazi.

Rais wa Shirikisho hilo Luis Rubiales amesimamishwa kazi na Shirikisho la Soka duniani (Fifa) baada ya kumbusu mshambuliaji Jenni Hermoso midomoni baada ya ushindi wa Kombe la Dunia la Wanawake la Uhispania.

Hermoso, 33, amesema busu baada ya mechi ya Jumapili iliyopita haikuwa ya maafikiano. Maria Dolores Martinez Madrona, mjumbe wa ulinzi wa itifaki hiyo, alisema suala hilo sasa linachunguzwa.

"Kama mjumbe wa ulinzi dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, jukumu langu ni kuzingatia itifaki na kulinda usiri wa wale walioathiriwa na tukio hili na Kamati ya Ushauri kuhusu masuala ya Unyanyasaji wa Kijinsia." alisema katika barua iliyochapishwa na shirikisho (RFEF).

Kifungu hicho huanza kufanya kazi mara tu malalamiko yanapowasilishwa na kamati ya ulinzi, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na mwamuzi wa kike Madrona, itachunguza na kutuma matokeo yake kwa Kamati ya Ushauri ya Unyanyasaji wa Kijinsia.

RFEF pia imeyaita mashirikisho ya kikanda kwenye mkutano "wa dharura" siku ya Jumatatu "kutathmini hali ambayo shirikisho hilo imekutana nayo". Ilipotangaza kuwa imemsimamisha Rubiales siku ya Jumamosi, Fifa iliiamuru RFEF na maafisa wake au wafanyakazi wasijaribu kuwasiliana na Hermoso, ambaye REFF ilikuwa imetishia kumchukulia hatua za kisheria mapema siku hiyo.

Licha ya ukosoaji mkubwa na shinikizo la kujiuzulu, Rubiales mwenye umri wa miaka 46 aliapa "kupigana hadi mwisho" wakati akihutubia mkutano mkuu usio wa kawaida ulioitishwa na RFEF siku ya Ijumaa.

Chanzo: Bbc