Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema ubora wa Luis Miquissone na Aubin Kramo unamuongezea upana wa kikosi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa na African Super League.
“Nimetoa nafasi kwa wachezaji wote ili kupata nafasi ya kuona uwezo wa kila mmoja. Nafurahi kuona Miquissone ameanza kuonyesha uwezo mzuri kama leo nimempa dakika zote na ameonyesha kiwango bora.
“Kwa upande wa Kramo licha ya kuingia kipindi cha pili kwenye mechi zote mbili za kirafiki, pia amenipa kitu kikubwa akifunga mabao mawili. Nitaendelea kumpa nafasi zaidi ili kuwa bora zaidi ya alipo sasa,”
“Ni mchezaji mzuri lakini bado naendelea kumpa muda zaidi ili apate uzoefu wa ligi ya Tanzania. Tayari nimeanza kumpa dakika chache kwenye mechi za kirafiki na ameonyesha uwezo mkubwa kwani ni miongoni mwa wachezaji watakaocheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na naamini watatusaidia,” amesema Robertinho.