Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Luis: Kaeni chonjo

Luis Miquison Pic 2 Data Luis: Kaeni chonjo

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limetangaza kikosi chake cha wiki kutokana na mechi mbalimbali ambazo zilichezwa katika mzunguko wa nne kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kikosi cha Simba ambacho katika mzunguko wa nne kilishinda mabao 3-0 katika uwanja wa nyumbani, Dar es Salaam dhidi ya Al Merrikh ya Sudan kimetoa wachezaji wawili kwenye timu hiyo bora ya wiki.

Wachezaji hao ni beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na mshambuliaji Luis Jose Miquissone ambaye ametamka kwamba ndio kwanza anaanza kuonyesha moto na mengi mazuri yanakuja.

Miquissone ambaye aliifungia Simba bao la kuongoza katika mchezo huo anaingia katika kikosi hicho kwa mara ya pili mfululizo baada ya awamu ya mwisho kuchaguliwa tena alipowafunga Al Ahly. Mchezaji mwingine alikuwa Joash Onyango.

Mwanaspoti lilimtafuta Miquissone na akasema: “Binafsi nitaendelea kupambana na kujituma zaidi ili kuisaidia timu yangu kupata matokeo mazuri katika kila mechi ili kufikia malengo ya kufika mbali katika mashindano haya.

“Najua nikifanya hivyo itakuwa nzuri kwa upande wangu, kwanza

Related Luis Miquissone awaacha kwenye mataa TP Mazembe

Kagere avunja ukimya Simba Simba baba lao miaka 5 ya Magufuli



UCHAMBUZI: Yanga wasijitoe kwenye reli ya ubingwa wa ligi kuunitaonekana kama mchezaji ambaye nafanya vizuri na fursa nyingi zitafunguka ikiwemo tuzo hizi za mchezaji bora wa wiki na nyinginezo nyingi.

“Tuzo hizo za CAF zinaongeza morali ya kufanya vizuri kwangu katika kila mechi kwani natamani kuzipata mara kwa mara, zitaongeza wasifu katika maisha yangu ya soka,” alisema Miquissone ambaye Mwanaspoti linajua ana dili za Morocco, Misri, Algeria na Afrika Kusini.

Timu hiyo ya wiki ambayo imechaguliwa na CAF ina wachezaji Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Diogenes Joao (Atletico Petroleos de Luanda), Tshabalala, Mosa Lebusa (Mamelodi Sundowns) na Mouad Haddad (MC Algiers).

Wengine Yasser Ibrahim (Al Ahly), Mehdi Benaldjia (MC Algiers), Lebohang Maboe (Mamelodi Sundowns), Hamdou Elhouni (Esperance Tunis), Mohamed Magdy (Al Ahly) na Miquissone.

Bao bora la wiki lilikwenda kwa mshambuliaji wa Al Ahly, Mohamed Afsha ambaye alilifunga katika mechi ya ugenini dhidi ya AS Vita jijini Kinshasa, DR Congo.
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz