Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Luis, Chama wazua jambo

Chama X Mquissone Luis, Chama wazua jambo

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati dirisha la usajili ukizidi kushika kasi kwa klabu mbalimbali kufukuzia na kuwasainisha majembe mapya, taarifa za viungo washambuliaji Clatous Chama na Luis Miquissone wameshtua na kuwa gumzo kwa mashabiki wa Yanga na Simba jijini Mbeya wametambiana kina kona.

Hali hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa tetesi za Chama kutikisa kiberiti Msimbazi kabla ya mabosi wa Simba kuingilia kati baada ya kuhusishwa na Yanga, huku Luis ikielezwa muda wowote kurejea kikosini kwa Wekundu na kurejeshas ile fleva ya misimu miwili iliyopita ya Simba.

Mastaa hao vipenzi vya mashabiki wamekuwa na kiwango bora uwanjani huku wakiisaidia Simba kwa nyakati tofauti na sasa wameonekana kuwateka mashabiki wa timu hizo kila upande ukitaja majina hayo.

Salum Mwampashi shabiki lialia wa Yanga alisema iwapo tetesi za Chama kutua kikosini humo zitatimia, anaona dalili za timu hiyo kutesa michuano ya ndani na nje akiungana na mastaa wengine.

Alisema Chama ni moja ya wachezaji bora wenye uwezo na kipaji cha soka na mara nyingi amekuwa akiwapa maumivu Yanga kutokana na uchezaji wake wakimtamani muda mrefu kutua Jangwani.

"Tunaomba sana tetesi ziwe uhalisia halafu akutane na mastaa wa Jangwani lazima mtu aumie, msimu ujao ni kama unachelewa kuanza Chama tunamtaka sana kikosini tuendelee kuwapa mauimivu watani," alitamba Mwampashi, bila kujua kwamba dili hilo la Chama ni kama limekufa.

Kwa upande wake Charles Beno shabiki kindaki ndaki wa Wekundu, alisema Simba haiwezi kumuachia Chama kutokana na mchango alionao kikosini, lakini iwapo Luis atarejea tena ndani itakuwa balaa msimu ujao.

“Hakuna ambaye hajui kazi ya Chama pale Msimbazi, anawatesa wengi na sidhani kama atauzwa kwenda Yanga haiwezekani, lakini taarifa za Luis kurejea Simba ni habari njema na ikiwa hivyo tutatesa sana,” alisema Beno. Dirisha likiendelea

Chanzo: Mwanaspoti