Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lozano ang’oka jino baada ya kugongana na Ndidi

Lozano And Ndidi  696x392 Lozano apata majeruhi

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Napoli Hirving Lozano alilazimika kutolewa uwanjani kwa machela ndani ya kipindi cha kwanza baada ya kugongana vibaya na Wilfred Ndidi wa Leicester City wakati wa mchezo wa Europa League.

Lozano alikuwa akikimbia na mpira na kujigonga kwenye mguu wa wa Ndidi na kichwa chake kujipigiza kwenye goti la Ndidi tukio lililopelekea kung’oa jino lake. Tukio kama hilo, kwa bahati mbaya, ni sawa na jeraha alilopata kwenye Gold Cup akiwa na Mexico.

Mwamuzi haraka aliwaita madaktari machela hadi uwanjani na kutolewa nje ya uwanja.

Wakati wa mapumziko kwenye mechi ya Europa League, Napoli na Leicester zilikuwa sawa kwa mabao 2-2, huku timu hiyo ya Premier League ikitoka nyuma kwa mabao mawili. Lakini dakika ya 57 Eljif Elmas aliifungia Napoli bao la tatu na la ushindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live