Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lomalisa yupo fiti, aisubiria Medeama kwa Mkapa

Lomalisa Mutambala Ms.jpeg Lomalisa yupo fiti, aisubiria Medeama Dar

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kuukosa mchezo wa leo wa ugenini dhidi ya Medeama wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huko Kumasi, Ghana, beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa atakuwa tayari kuitumikia timu yake katika mechi ya marudiano baina ya timu hizo itakayochezwa Desemba 20 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Beki huyo alipata majeraha ya enka katika mchezo uliopita wa Yanga dhidi ya Al Ahly kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao timu yake ilitoka sare ya bao 1-1 ambao alishindwa kumaliza na kumpisha Nickson Kibabage.

Lomalisa alimpisha Kibabage katika dakika ya 36 baada ya kufanyiwa faulo na Percy Tau wa Al Ahly na daktari wa Yanga, Moses Etutu amethibitisha kuwa majeraha hayo yatamuweka nje kwa wiki moja hivyo atakuwepo uwanjani kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Al Ahly.

"Hakupata majeraha makubwa yalikuwa ni ya wastani tu. Aliweza kubaki nyumbani (Tanzania) ilikuweza kuendelea na matibabu ya kawaida ili kusaidia kurejea katika hali yake ya kawaida na kupona kwake kuwe kwa haraka na baada ya wiki moja tu atakuwa tayari kucheza.

"Kiujumla wachezaji wote waliosafiri kuja hapa Ghana ni wazima na tunashukuru Mungu hakuna majeraha makubwa yanayoweza kumzuia mchezaji kucheza mechi hii (dhidi ya Medeama) na linabakia kuwa suala la kocha kuamua nani acheze na nani asicheze," alisema Etutu.

Daktari huyo alisema kuwa jana walipanga kufanya program za kuchua misuli na masaji ili kuwaweka wachezaji wao katika hali nzuri kimwili tayari kwa mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Baba Yara, Kumasi.

Akizungumzia mchezo wa leo, beki wa Yanga, Dickson Job alisema wana nafasi kubwa ya iwapo kila mchezaji atatimiza wajibu wake uwanjani.

"Hii ni mechi ngumu lakini sisi Yanga tuna ubora wetu sio kitu kipya kwetu kuweza kushinda ugenini hata hii mechi mimi tunatakiwa kufunga mabao ya kutosha."

"Mabeki tumejipanga sawasawa hatutaki kuyarudia makosa ya nyuma timu nzima ilicheza vizuri mechi iliyopita tunataka umakini ule uongezeke," alisema Job.

Kwa upande wa meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema kuwa mazingira ya kambi yao ni salama na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kwa ajili ya mechi ya leo.

"Timu imefanya mazoezi vizuri na program zinaenda kama zilivyopangwa. Tunaushukuru uongozi kwa kuandaa mazingira mazuri hapa na tuna imani tutafanya vizuri," alisema Harrison.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: