Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lomalisa huyooo! Kutua zake Azam FC

Lomalisa Mutambala Ms.jpeg Beki wa kushoto wa klabu ya Yanga, Joyce Lomalisa.

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kushoto wa klabu ya Yanga, Joyce Lomalisa inaelezwa anakaribia kumalizana na klabu ya Azam FC kwa ajili ya kuichezea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa Azam FC kimesema mazungumzo baina ya mchezaji huyo yanaendelea vizuri na muda wowote kuanzia sasa watamtangaza mchezaji huyo kuwa mali yao. 

"Mazungumzo baina ya Lomalisa na uongozi yamefikia hatua ya nzuri na wanaelekea kuafikiana, naamini wakikubaliana atasaini kwa ajili ya kujiunga na timu yetu msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.  

Alisema Azam msimu ujao imepania kufanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na yale ya kimataifa na ndio sababu ya kuboresha kikosi chao. 

"Malengo yetu ni kufanya vema msimu ujao, tunaamini usajili tutakaoufanya utaiboresha timu yetu na kushika nafasi za juu,” kilisema chanzo hicho. 

Lomalisa alikuwa sehemu ya mafanikio ya klabu ya Yanga msimu huu baada ya kuisaidia kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live