Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lomalisa alia na mabosi Yanga

Bangala X Lomalisa Lomalisa alia na mabosi Yanga

Sat, 20 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kupata dili la kuichezea G.D. Sagrada Esperanca ya Angola, beki wa kushoto aliyeachwa Yanga, Joyce Lomalisa amelia na mabosi wa klabu hiyo ya Jangwani kwa kumwekea kauzibe kupata ofa nzuri kwa timu zilizokuwa zikimpigia hesabu kumsajili kabla ya Waangola hao kumrudia katika Ligi ya Girabola.

Lomalisa alisema alikuwa anatamani sana kusalia Jangwani, lakini mambo yalitibuka na kinachomuuma ni kuchelewa kupatikana kwa muafaka wa kuachwa aondoke kuliko mkosesha dili nyingi.

Beki huyo aliyeitumikia Yanga kwa misimu miwili, amejiunga na Sagrada Esperanca, aliyokuwa akiitumikia kabla ya kujiunga na Yanga, pia akiwahi kuitumikia Inter Club pia ya huko huko Angola mbali na AS Vita kwa DR Congo anakotokea nyota huyo.

Akizungumza na Mwanaspoti Lomalisa alisema, amerudi Angola kwa kuwa ni kama nyumbani kwake japo alitamani kubaki Tanzania.

“Yanga walinionyesha nia ya kunibakisha nikapotezea ofa, wakageuka.”

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: