Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lomalisa: Mziki wa kina Pacome, Yao si mchezo

Lomalisa Mutambala Ms.jpeg Beki wa Yanga, Joyce Lomalisa

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Yanga, Joyce Lomalisa amesema ujio wa Pacome Zouzoua, Attohoula Yao umechangia kwa kiasi kikubwa timu yao kutwaa taji la tatu mfululizo ambalo ni la 30 tangu wameanza kushiriki Ligi Kuu Bara.

Lomalisa ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu ametwaa mataji mawili ndani ya Yanga katika misimu ya 2022/23 na 2023/24, ameiambia Mwanaspoti kuwa ongezeko la mastaa hao katika dirisha kubwa la usajili lililopita ni chachu ya kutetea taji.

"Ubora tuliokuwa nao msimu uliopita pia ungeweza kutetea taji, lakini sio kwa mafanikio haya makubwa kwani wachezaji wengi tayari walikuwa wamevuja jasho sana, hivyo wangekuwa na 'fatiki' tofauti na walipoongezwa kina Maxi Nzengeli, Pacome na Yao," amesema Lomalisa.

"Kuongezwa kwao kuliongeza nguvu kikosini na kuifanya timu kuwa na usawa na wao kuna kazi kubwa wameifanya ili tuweze kutetea taji naweza kusema msimu huu ulikuwa bora zaidi ya msimu uliopita."

Lomalisa amesema ubora wa kikosi unatokana na namna timu inavyoshirikiana, huku akiweka wazi kuwa Yanga ni bora kila eneo na haimtegemei mtu kama ilivyokuwa msimu uliopita chini ya kocha Nasreddine Nabi.

"Msimu uliopita chini ya Nabi kulikuwa na utegemezi ukimkosa Fiston Mayele na Khalid Aucho timu inayumba na kupotea kwenye nafasi wanazocheza, lakini msimu huu tunaoumaliza kila mchezaji ana umuhimu na anatoa mchango wake kwa usahihi," amesema.

"Najivunia kuwa na misimu miwili ya mafanikio ndani ya Yanga kila mchezaji anandoto ya kunyanyua mataji kwenye timu anayoenda hilo kwangu limefranikiwa kwa asilimia kubwa nimecheza timu yenye mafanikio makubwa licha ya kushindwa kufanya vizuri kimataifa."

Lomalisa amesema pamoja na kushindwa kutwaa mataji ya kimataifa wameonyesha ushindani mkubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu na uliopita ambao walifika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, hatua ambazo timu hiyo kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita ilikuwa haijawahi kufika.

"Sijatwaa mataji ya kimataifa, lakini najivunia kuwa miongoni mwa wachezaji walioandika historia msimu wa kwanza nimecheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika na nimefikisha timu hatua ya riobo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika," amesema.

"Ni rekodi ambayo wachezaji wengi waliopita Yanga walishindwa kuifikia mimi miaka miwili tu nimekuwa sehemu ya mafanikio hayo hivyo naweza kusema nimecheza kwa mafanikio makubwa na najivunia hilo."

Lomalisa amewahi pia kuzicheza AS Vita ya DR Congo, Mouscron (Ubelgiji), GD Interclube na Bravos do Maqui zote za (Angola).

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: