Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lolote linaweza kuwakuta!

Erik Ten Hag Manchester United September 2023 1 Kocha wa Man United, Erik Ten Hag

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ghafla tu Erik ten Hag ameingia kwenye orodha ya makocha wanaoweza kufunguliwa mlango wa kutokea mapema kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Lakini, hadi sasa zikiwa zimechezwa mechi sita, kocha wa Sheffield United ndiye ambaye anaripotiwa kuukaribia zaidi mlango ulioandikwa exit kutokana na timu hiyo kuwa na matokeo ya hovyo kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England.

Hii hapa orodha ya makocha 10 kwenye Ligi Kuu England ambao lolote linaweza kuwakuta linapokuja suala la uwezekano wa kupigwa chini kwa matokeo ya hovyo.

1) Paul Heckingbottom (Sheffield United)

Tayari jina lake liliwekwa kwenye orodha ya wanaoweza kufukuzwa kabla hata hajachapwa 8-0 nyumbani. Kocha huyo alikuwa kwenye wakati mgumu wakati kikosi chake kilipokubali kipigo hicho kizito kutoka kwa Newcastle United. Huenda mabosi wanaweza wasichukue uamuzi kutokana na kufungwa na timu hiyo, lakini Heckingbottom hatakuwa salama kama timu hiyo itapigwa tena, hasa kutokana na Chris Wilder kupigiwa hesabu za kuja kuchukua mikoba yake.

2) Gary O’Neil (Wolves)

Ni kitu kinachoshangaza kwamba kumwona kocha aliyeonekana anafaa na kupewa kazi naye amewekwa kwenye orodha ya wanaoweza kufunguliwa mlango wa kutokea. Kocha Gary O’Neil anashika namba mbili kwenye orodha ya makocha wanaoweza kufukuzwa kazi kutokana na mwenendo wa kikosi hicho kwenye Ligi Kuu England. Wolves inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamekusanya pointi nne katika mechi sita, huku wakiwa wamepoteza mechi nne kati ya sita walizocheza.

3) Sean Dyche (Everton)

Presha inapanda na kushuka kwa kocha Sean Dyche kwenye kikosi chake cha Everton. Mambo yake si matamu sana kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Timu hiyo inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, ikiwa imevuna pointi nne tu katika mechi sita. Mwenendo wa ndani ya uwanja wa timu yake ndicho kitu kinachomfanya awekwe kwenye namba tatu katika orodha ya makocha wanaoweza kufukuzwa kazi mapema kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

4) Mauricio Pochettino (Chelsea)

Mambo si mambo kwa upande wa Pochettino huko Chelsea. Kikosi hicho kimeshindwa kupata bao dhidi ya Nottingham Forest, Bournemouth na Aston Villa kitu ambacho kinamweka kocha huko kwenye wakati mgumu kwelikweli. Kuna wasiwasi kama Pochettino ataendelea kuwa kocha wa Chelsea hadi itakapofika Novemba 6 ambapo watakuwa na mechi ya Tottenham. Chelsea itakuwa kwenye wakati mgumu wa kumenyana na Arsenal, Brentford, Tottenham, Man City, Newcastle, Brighton na Man United.

5) Erik ten Hag (Man United)

Tangu msimu huu wa Ligi Kuu England ulipoanza, Manchester United imekuwa na mwenendo wa hovyo jambo linalomfanya kocha Erik ten Hag kuwa kwenye hatari ya kuwa mmoja wa makocha wanaoweza kupoteza ajira zao mapema. Ushindi dhidi ya Burnley wa Jumamosi umepunguza presha kwa kocha huyo baada ya kupoteza kwenye mechi tatu mfululizo. Hata hivyo, mechi hiyo bado haiwi kipimo cha kumfanya Ten Hag awe salama, vichapo vingine zitamweka kwenye hatari kubwa ya kufutwa kazi.

6) Rob Edwards (Luton)

Mechi tano pointi moja si mwendo mzuri kabisa wa Luton kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Kocha, Rob Edwards atakuwa kwenye wakati mgumu kwenye kibarua chake kutokana na timu hiyo kushindwa kupata matokeo mazuri ambapo hadi sasa kumekuwa na wasiwasi kama wataweza kupata pointi za kuwafanya wasishuke daraja. Kwa sasa Luton wanaweza wasifikirie kumfukuza kazi Edwards, lakini kama matokeo yatazidi kuwa mabaya, mlango wa kutokea utamhusu.

7) Marco Silva (Fulham)

Kocha, Marco Silva aligomea ofa ya pesa nyingi ya kwenda kufanya kazi huko Saudi Arabia, lakini tayari amewekwa kwenye nafasi ya saba ya makocha wanaoweza kufunguliwa mlango wa kutokea mapema kwenye Ligi Kuu England. Fulham mambo yake si mazuri, ikiwa imevuna pointi nane kwenye mechi sita. Marco Silva anaweza kuwa salama kwa wakati huu, lakini kwa timu ya aina ya Fulham inayohitaji pointi za mapema kujiweka sawa isishuke daraja, kocha huyo atakuwa hatarini.

8) Andoni Iraola (Bournemouth)

Moja ya makocha wageni kwenye Ligi Kuu England kwa msimu huu. Kwa sasa bado yupo kwenye nafasi za mbali kwa makocha wanaoweza kufukuzwa kazi, lakini jina lake limo kwenye wale 10 wa mwanzo, ambao chochote kinaweza kutokea kwenye ishu ya kufunguliwa mlango wa kutoka kwenye kikosi cha Bournemouth. Iraola ni moja ya makocha wanaoonyesha viwango vizuri, lakini kila kitu kitabebwa na uwezo wake wa uwanjani katika kuhakikisha timu yake inavuna pointi za kuwafanya wasishuke.

9) Steve Cooper (Nottingham Forest)

Pointi saba kwenye mechi sita si rekodi nzuri sana kwa Nottingham Forest. Jambo hilo linamfanya kocha wao Steve Cooper kuwa kwenye orodha ya makocha waliopo katika nafasi kubwa ya kuonyeshwa mlango wa kutokea. Forest si timu nyepesi sana na kama itafanikiwa kupata pointi za kubaki kwenye Ligi Kuu England basi jambo hilo litamfanya kocha Cooper kuwa salama, lakini kinyume cha hapo basi chochote kinaweza kumkuta.

10) Vincent Kompany (Burnley)

Alihusishwa na klabu kubwa kibao baada ya kuonyesha makali wakati anaisaidia Burnley kurejea kwenye Ligi Kuu England. Lakini baada ya kufika kwenye ligi, mambo yamekuwa tofauti kabisa.

Chanzo: Mwanaspoti