Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lokosa wa okosa wa Simba atua, imba atua, Fiston leo

F9960451e66461d4b2cc51ce40f19f33 Lokosa wa okosa wa Simba atua, imba atua, Fiston leo

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Nigeria, Junior Lokosa ametua nchini jana kumalizana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba huku mshambuliaji mpya wa Yanga, Fiston Abdoul Razak akitarajiwa kutua Dar es Salaam leo.

Lokosa alikuwa kivutio kikubwa kutokana na wingi wa mabegi aliyokuja nayo, kwani alikuwa na mabegi manne, makubwa mawili na madogo mawili.

Lokosa mwenye umri wa miaka 27 ana uzoefu na soka la Afrika ambapo amewahi kucheza nchini Nigeria na Tunisia katika klabu za Esperance, Kano Pillars na First Bank.

Simba imekuwa ikiboresha kikosi chake kwa ajili ya kujipanga na hatua ya makundi michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipokelewa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Dk Arnold Kashembe baada ya kutua kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kusema: “Ninao uzoefu wa kucheza mashindano haya makubwa lakini hata kucheza klabu kubwa kama Esperance Sportive de Tunis naimani hilo nitakuja kuliongeza katika timu hii ili kufanya vizuri,” alisema.

“Ndio kwanza nimefika hapa nchini siwezi kusema mambo mengi ila muda ambao nitakuwepo hapa na mechi ambazo nitacheza kila mtaona,” alisema Akiwa katika klabu ya Kano Pillers msimu wa 2017/2018 aliifungia timu hiyo mabao 23 katika michezo 35 aliyocheza.

Lokosa ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Simba katika kipindi cha dirisha dogo baada ya Perfect Chikwende, Gikanji Doxa na Taddeo Lwanga.

Hii inamaanisha Simba itakuwa na washambuliaji wanne. Baada ya Lokosa wengine ni John Bocco, Meddie Kagere na Chris Mugalu. Katika hatua nyingine wachezaji wote wa Simba ambao hawako katika timu zao za taifa, juzi jioni waliwasili kambini na jana walianza mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi, Ligi ya mabingwa Afrika na Kombe la Simba.

Pia Simba imemalizana na kocha wa makipa, Milton Nienov kutoka Brazil baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili. Wachezaji wote wapya watatambulishwa kwenye michuano maalumu waliyoiandaa ya Simba Super Cup itakayo- fanyika kuanzia Jumatano na kushirikisha klabu tatu za TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo na Al Hilal ya Sudan na wao wenyewe.

Licha ya dirisha dogo kwa upande wa Tanzania kufungwa Januari 15 Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limezipa nafasi timu zinazocheza michuano hiyo ya kimataifa kuendelea kusajili.

Naye Ofisa mhamasishaji wa klabu ya Yanga, Antonio Nugaz alisema mchezaji Fiston atawasili saa 10 jioni lakini awamu hii hawatafanya mapokezi makubwa kama ilivyozoeleka kwa wachezaji kadhaa waliopita.

“Mchezaji atatua kesho (leo) na kujiunga na wenzake katika kambi ya maandalizi ya ligi, hatutegemei kufanya mapokezi makubwa kama ilivyozoeleka,”alisema.

Fiston atajiunga na wenzake wanaotarajiwa kuingia kambini kuanzia kesho kujiandaa na ligi kuu. Fiston ni miongoni mwa wachezaji watatu waliosajiliwa na klabu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili lililofungwa hivi karibuni.

Wengine ni Saido Ntibazonkiza na Dickson Job. Yanga ipo kileleni ikiwa na pointi 44 katika michezo 18, ikiwa haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa zaidi ya kupata sare moja.

Chanzo: habarileo.co.tz