Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yazidi kupukutika kwa majeruhi, Matip, Arnold nje wiki mbili

Matip Joel X Arnold.jpeg Joel matip x Arnold watakua nje kwa wiki mbili

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabeki wa klabu ya Liverpool Joel Matip na Trent Alexender Arnold wanatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili kila mmoja.

Wachezaji hao wanaelezwa kua nje ya uwanja kwa mda wa wiki mbili huku Joel Matip habari zinaeleza anaweza kua nje hadi wiki tatu kutoka na majeraha ya ambayo yanamkabili.

Trent Alexender Arnold alitolewa baada ya kipindi cha kwanza kumalizika katika mchezo uliomalizika kwa klabu ya Liverpool kupoteza kwa mabao 3-2 siku ya Jumapili ambapo pia Matip alitolewa katika mchezo huo.

Joel Matip ambae amekua akipata majeraha ya mara kwa mara katika timu hiyo ambapo wakati msimu unaanza alikua anauguza majeraha ila wakati amerudi akiwa hajacheza mechi hata tano amepata majeraha kwa mara nyingine.

Liverpool inapitia kipindi kigumu sana tangu kuanza kwa msimu huu wakipata matokeo mabaya huku wakiandamwa na wimbi la majeruhi kwa wachezaji wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live