Klabu ya Liverpool imewaonya mashabiki wake waliosafiri kwenda jijini Napoli kwa ajili ya kutazama mchezo wa ligi ya Mabingwa kati ya timu yao na mwenyeji wao Napoli baada ya vitisho vya mashabiki wa klabu hiyo.
Mchezo wa kati ya Liverpool na Napoli unatarajiwa kuchezwa leo jumatano kwenye dimba la Stadio Diego Armando Maradona kwenye majira ya saa nne kamili usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.
Klabu ya Liverpool iliachia waraka wake wa kuwataadharishaha mashabiki wa timu hiyo ambao watasifiri kwenda nchini italia na pia iliwataka mashabiki wake wasivae jersey za timu wanaposafiri kuelekea nchini Italia.
“Mashabiki hawapaswi kukusanyika kwenye maeneo ya wazi ili kuepuka kutengwa kwenye maeneo ya bandari ndani jiji.
“Tunapendekeza mashabiki kujiepusha kwenye maeneo ya katikati ya jiji. Ikiwa utachagua kutembelea, tafadhali kuwa makini unaweza kuwa miongoni mwa watu kuwa kwenye hatari ya kuibiwa, kuporwa na kunyanyaswa.”
Klabu ya Liverpool imetoa waraka huo kutokana na mashabiki wa klabu ya Napoli kutangaza kuwafanyia vitendo visivyofaa mashabiki wa klabu wataosafiri kwa ajili ya kutazama mchezo huo.