Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yatoa 'Thank You' kwa mastaa 10, Thiago yumo

Matip X Thiago Liverpool yatoa 'Thank You' kwa mastaa 10, Thiago yumo

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Liverpool imetangaza kuwatema wachezaji 10 wakiwamo masupastaa, Joel Matip na Thiago Alcantara.

Miamba hiyo itaondoka Anfield kutokana na mikataba yao kufika ukingoni. Matip na Thiago walipewa nafasi ya kuaga kwenye mchezo wa mwisho wa msimu ambapo Liverpool ilikipiga na Wolves, ambapo ilikuwa mechi ya mwisho pia kwa kocha Jurgen Klopp.

Kwa mastaa wanaoondoka Liverpool orodha yake haikushia kwa hao tu baada ya miamba hiyo kuwafungulia mlango wa kutokea Adam Lewis na Melkamu Frauendorf, ambao walipewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza na kocha Klopp.

Mateusz Musialowski, alicheza dhidi ya Sparta Prague mapema msimu huu, naye yumo kwenye orodha hiyo watakaoondoka, huku wengine ni Nathan Giblin, Francis Gyimah, Luke Hewitson, Niall Osborne na Cody Pennington.

Taarifa ya klabu ya Liverpool, ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha Arne Slot ilifichua hivi: “Kila mtu hapa Liverpool FC anawashukuru Joel, Thiago, Adam, Melkamu, Mateusz, Nathan, Francis, Luke, Niall na Cody kwa mchango wao na tunawatakia kila la heri huko waendako.”

Wakati kukiwa na orodha hiyo ya wanasoka wanaoondoka, Liverpool ipo kwenye mchakato wa kuwasainisha mikataba mipya mastaa wake.

Kipa Mhispaniola, Adrian amepewa ofa mpya ya kuendelea kubaki kwenye kikosi.

Makipa wa kutokea kwenye akademia, Jacob Poytress na Reece Trueman nao watabaki Anfield. Na kitakachofuata baada ya hapo ni kocha Slot kuanza kusajili wakali wapya kwenye dirisha hili.

Kutahitajika wachezaji wakuja kuziba mapengo ya Matip na Thiago. Beki Mcamerooni, Matip alisema:

“Imekuwa miaka minane ya furaha kubwa Liverpool. Niliruhusiwa kuwa sehemu ya historia ya klabu hii chini ya kocha bora kabisa. Tumefanikiwa kubeba mataji makubwa kabisa. Mimi na mke wang tunawashukuru sana kwa sapoti yetu pamoja na watoto wetu. Mtabaki kwenye kumbukumbu zetu daima.”

Chanzo: Mwanaspoti