Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yatinga Nusu Fainali Carabao Cup

Liverpool Vs Leicester Highlights Scaled Diogo Jota akiifungia Liverpool goli la Pili

Thu, 23 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majogoo wa Jiji, Timu ya Liverpool imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 3-3 na Leicester City usiku huu Uwanja wa Anfield.

Mabao ya Leicester City yamefungwa na mshambuliaji mkongwe, Jamie Vardy mawili, dakika ya tisa na 13 na James Maddison dakika ya 33, wakati ya Liverpool yamefungwa na Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 19, Diogo Jota dakika ya 68 na Takumi Minamino dakika ya 90 na ushei.

Katika mikwaju ya penalti, sifa zimuendee kipa wa pili wa Liverpool, Caoimhin Kelleher aliyeokoa mikwaju miwili ya wachezaji wa Leicester City, Luke Thomas na Ryan Bertrand.

Minamino pekee alikosa penalti upande wa Liverpool, wakati wote, James Milner, Roberto Firmino, Oxlade-Chamberlain, Naby Keïta na wote walifunga.

Waliofunga Penalti za Leicester City ni Youri Tielemans, James Maddison, Marc Albrighton na Kelechi Iheanacho na sasa Wekundu hao watakutana na Arsenal katika Nusu Fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live