Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yatanguliza mguu mmoja robo Fainali UEFA

Liverpoolsalah Mshambuliaji wa Liverpool, Mohammed Salah

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool imefunga goli mbili za jioni na kuondoka na ushindi wa goli 2-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora baina yao na wenyeji Inter Milan mchezo uliopigwa dimba la San Siro Italia.

Liverpool kwa kipindi kirefu kwenye mechi hiyo imetumia kukaba ambapo magoli yake yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Roberto Firmino akimalizia mpira wa kona wa Andrew Robertson.

Bao la pili likafungwa na nyota wa Misri Mohamed Salah baada ya makosa ya kiulinzi ambayo yametokea kwenye eneo la Ulinzi.

Kwa matokeo hayo, Liverpool itakuwa inahitaji kushinda, sare au hata kufungwa chini ya goli moja katika mchezo wa marudiano ili kufuzu kucheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live