Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yatafuta kocha spesho wa mipira ya kutenga

Liverpool Liver Liverpool yatafuta kocha spesho wa mipira ya kutenga

Tue, 21 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Liverpool imetoa tangazo la kutafuta kocha wa mipira ya adhabu wa kuja kufanya kazi chini ya kocha mpya, Arne Slot huku tangazo hilo la kazi likitangazwa LinkedIn.

Liverpool inajipanga kuanza maisha mapya baada ya kuagana na kocha wao Jurgen Klopp.

Kocha Slot, 45, ameshathibitishwa atakuja kurithi mikoba ya Mjerumani huyo na ataanza kazi rasmi mwezi ujao.

Kocha huyo Mdachi alifanya vizuri kwenye klabu ya Feyenoord alipofanya kazi kwa miaka mitatu na sasa yupo kwenye kazi ya kuboresha benchi lake la ufundi wakati akielekea huko Anfield.

Makocha waliokuwa chini ya Klopp, Pep Ljinders na John Achterberg nao wataondoka, huku Slot ataandamana na msaidizi wake Sipke Hulshoff, lakini kwa sasa wanahitaji kocha wa mipira ya adhabu.

Tangazo hilo linaelezea vigezo vya mtu wanayemtaka ili aje kufundisha mipira ya adhabu iwe na maana kubwa kwa msimu ujao.

Mshahara ni mzuri na kutakuwa na likizo ya siku 25 na michango kwenye mifuko ya jamii. Atakayebahatika kupata kazi hiyo atakwenda kufanya kazi uwanja wa mazoezi wa timu hiyo wa AXA Training Ground.

Licha ya klabu nyingi za Ligi Kuu England kutumia makocha wenye ujuzi wa kupiga mipira ya adhabu, Liverpool ilikuwa na kocha mmoja, aliyekuwa akijihusisha na hilo chini ya Klopp, ambaye alikuwa msaidizi, Peter Krawietz.

Liverpool imenasa huduma ya Slot baada ya kulipa fidia ya kuvunja mkataba wake Feyenoord kwa ada ya Pauni 9.4 milioni na Jumatatu ilimtangaza Mdachi huyo ndiye mrithi rasmi wa Klopp.

Chanzo: Mwanaspoti