Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liverpool yapata pigo, Diaz apata majeraha mapya

C7FA9695 FA25 4A48 AE64 F0536A8F8CA1.jpeg Luis Diaz apata majeraha kambi ya Liverpool Dubai

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maandalizi ya Liverpool kurejea Ligi Kuu ya Uingereza yamepata pigo kubwa kwa Luis Diaz kurudishwa kutoka kambi yao ya mazoezi ya Dubai akiwa majeruhi.

Winga huyo wa Colombia alijeruhiwa goti wakati wa kichapo cha 3-2 dhidi ya Arsenal mwezi Oktoba, suala ambalo Jurgen Klopp alitarajia lingechukua miezi mitatu kupona.

Liverpool walifarijika wakati huo kwamba hakuwa amejeruhiwa kwenye nyama za mbele na aliepuka upasuaji.

Diaz alikuwa akiendelea vizuri wakati wa matibabu yake na alikuwa akifanya mazoezi mepesi katika siku 10 kabla ya kusimama kwa Ligi Kuu.

Aliendelea kufanya mazoezi wakati wachezaji wa Liverpool ambao sio wa Kombe la Dunia walipewa likizo na alikuwa katika hali nzuri.

Ilitarajiwa kwamba angepata muda wa kucheza huko Dubai, ambapo Liverpool itamenyana na Lyon Jumapili na AC Milan Ijumaa ijayo, kujiandaa kwa mechi ya ufunguzi dhidi ya Manchester City kwenye Kombe la Carabao na Aston Villa Siku ya Boxing Day lakini mpango huo ni, sasa umesimama.

Hakuna ubishi kuwa hili ni pigo kubwa kwa Klopp, ambaye alimsajili Diaz Januari mwaka jana kutoka Porto na kumfanya kuwa mtu muhimu sana katika kipindi cha pili cha msimu uliopita, na kuisaidia Liverpool kushinda kombe la FA na Carabao.

Hadi sasa, hakuna dalili zozote zinazoonyesha ni muda gani Diaz atakaa nje ya uwanja au iwapo atahitaji kufanyiwa upasuaji lakini ukweli kwamba amerejea England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live